AU YATISHIA MAKUNDI HASIMU BURUNDI

AU YATISHIA MAKUNDI HASIMU BURUNDI

Like
248
0
Wednesday, 30 December 2015
Global News

UMOJA  wa  Afrika  leo  umetishia  kuyawekea vikwazo makundi  hasimu  nchini  Burundi  iwapo  yatashindwa kuhudhuria  mazungumzo  ya  amani  mwezi  ujao, wakati ukiibana  serikali   kukubali jeshi  la  kulinda  amani.

Serikali  ya  Burundi  na  upinzani, pande  zilizokutana nchini  Uganda  siku  ya  Jumatatu,  zinatarajiwa  kukutana tena  Januari  Mjini Arusha kwa  mazungumzo  yenye  lengo  la  kumaliza miezi  kadhaa  ya  ghasia.

Comments are closed.