AU YATOA HESHIMA ZA PEKEE KWA BABA WA TAIFA MWL. JK NYERERE

AU YATOA HESHIMA ZA PEKEE KWA BABA WA TAIFA MWL. JK NYERERE

Like
381
0
Tuesday, 03 February 2015
Local News

UMOJA wa Nchi Huru za Afrika –AU, umetoa heshima pekee kwa Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere na kumuenzi kwa kuamua kuwa moja ya majengo yake muhimu katika makao makuu ya Umoja huo mjini Addis Ababa, Ethiopia, litapewa jina la Mwalimu Julius Nyerere.

Mwalimu Julius Kambarage Nyerere anapewa heshima hiyo kubwa kwa mchango wake katika ukombozi wa Bara la Afrika na kuliondoa Bara hilo katika ukoloni.

Uamuzi wa kuliita Jengo la Baraza la Amani na Usalama (Peace and Security Council) la Umoja huo Mwalimu Julius Nyerere Hall ulifikiwa, wakati wa kikao cha ndani cha marais wa nchi wanachama wa AU kilichofanyika makao makuu ya Umoja huo mjini Addis Ababa.

 

Comments are closed.