AUA MKEWE KWA UGOMVI WA KIMAPENZI

AUA MKEWE KWA UGOMVI WA KIMAPENZI

Like
214
0
Friday, 21 August 2015
Local News

MTU mmoja ambaye hajafahamika jina lake mara moja mkazi wa wilaya ya Bagamoyo mkoani Pwani amemuua mke wake kwa kumchoma kisu sehemu tofauti za mwili kufuatia kuwepo kwa ugomvi wa muda mrefu baina yao.

 

Hali hiyo imetokana na kuwepo kwa sintofahamu baina ya wanafamilia hao suala ambalo awali lilifikishwa kituo cha polisi kilichopo wilayani hapo kwaajili ya kulitolea ufafanuzi.

 

Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo kamanda wa polisi mkoa wa Pwani ULRICH MATEI amesema kuwa tukio hilo limetokea katika ofisi za Bakwata wakati watu hao wakienda kupata muafaka wa matatizo yao.

 

Comments are closed.