AUA MKEWE NA KUMZIKA

AUA MKEWE NA KUMZIKA

Like
276
0
Friday, 27 February 2015
Local News

JESHI la Polisi Mkoa wa Kilimanjaro linamtafuta PETER MROSO mkazi wa Kijiji cha Ubetu Wilayani Rombo kwa tuhuma za kumuua mkewe kisha kuuzika mwili wake na kubakiza kichwa.

Tukio hilo limetokea February 25 mwaka huu nyumbani kwa Marehemu maeneo ya Ubetu ambapo mtuhumiwa alimpiga mkewe JENIPHER PETER  sehemu za kichwani.

Mashuhuda ambao hawakutaka kutaja majina yao wamedai kuwa mara baada ya mume huyo kumpiga mkewe hadi kufa aliuchukua mwili wake na kwenda kuuzika katika boma la ng’ombe huku kichwa chake kikibaki juu.

Comments are closed.