AUAWA KWA KUDAI MTOTO WAKE KWA MKE WA MTU

AUAWA KWA KUDAI MTOTO WAKE KWA MKE WA MTU

Like
254
0
Thursday, 22 October 2015
Local News

KATIKA tukio la kusikitisha, mkazi wa kitongoji cha Songambele Mji mdogo wa Mirerani Wilayani Simanjiro Mkoani Manyara, ameuawa kwa kukatwa katwa mapanga, baada ya kudai mtoto wake kwa mke wa mtu.

 

Wakizungumza kuhusiana na tukio hilo baadhi ya mashuhuda wamedai kuwa marehemu huyo alikuwa na uhusiano wa kimapenzi wa muda mrefu na mwanamke huyo ambaye ni mke wa mtu.

 

Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo, kamanda wa polisi wa mkoa wa Manyara, kamishna msaidizi (ACP) Christopher Fuime amesema tukio hilo limetokea jana saa 5 usiku kwenye kitongoji cha Songambele mji mdogo wa Mirerani.

Comments are closed.