AZAKI YAZINDUA ILANI YA UCHAGUZI

AZAKI YAZINDUA ILANI YA UCHAGUZI

Like
349
0
Monday, 07 September 2015
Local News

ASASI za kiraia nchini–AZAKI-imezindua ilani inayoakisi malengo yatakayoinufaisha jamii katika kipindi cha kuelekea na baada ya uchaguzi mkuu ujao ambayo itakuwa dira na mwongozo kwa wananchi na vyama vyote vya siasa.

Akifungua hafla hiyo ya uzinduzi jana katika mkutano na waandishi wa habari jijini Dar es salaam mwenyekiti wa tume ya haki za binadamu Bahame Tom Nyanduga amesema lengo la asasi hiyo ni kuhakikisha kunakuwa na kampeni za Amani na  uchaguzi usio wa vurugu.

Aidha Nyanduga ameongeza kuwa tume imejipanga vyema kusimamia misingi ya uchaguzi hivyo kwa yeyote atakayekiuka taratibu za uchaguzi na kusababisha uvunjifu wa haki za binadamu sheria itashika mkondo wake.

Comments are closed.