Azam Fc Yatolewa Cecafa Kagame Cup Kwa Penati

Azam Fc Yatolewa Cecafa Kagame Cup Kwa Penati

Like
917
0
Wednesday, 20 August 2014
Slider

Azam-

Timu ya soka ya Azam Fc ambayo ilikuwa inashiriki mashindano ya cecafa kwa timu za ukanda wa Africa Mashariki nchini Rwanda imeyaaga rasmi mashindano hayo jioni hii baada ya kufungwa na timu ya Sudan El marreikh kwa penati 4 kwa tatu.

Timu hizo ambazo zimekutana katika hatua ya robo fainali ya mashindano ya Cecafa Kagame Cup zilishindwa kufungana magolo ndani ya dakika 45 za kila upande na hivyo kuamuliwa zipige penati iliyoamua mshindi kati yao.

Mabao ya Azam ya penati ya Azam yalifungwa na Aggrey Morris, Didier Kavumbagu na Erasto nyoni huku mchezaji Leonel saint Preux  na Shomari Kapombe wakikosa penati zao.

 

Comments are closed.