AZERBAIJAN: KAMISHENI YA UMOJA WA ULAYA YAIDHINISHA UJENZI WA BOMBA LA KUSAFIRISHA GESI

AZERBAIJAN: KAMISHENI YA UMOJA WA ULAYA YAIDHINISHA UJENZI WA BOMBA LA KUSAFIRISHA GESI

Like
298
0
Friday, 04 March 2016
Global News

 

KAMISHENI ya Umoja wa Ulaya imeidhinisha makubaliano kati ya Umoja huo na Ugiriki juu ya ujenzi wa bomba la kusafirishia gesi kutoka Azerbaijan unaolenga kupunguza utegemezi wa nishati kwa Urusi.

Bomba hilo lenye urefu wa kilomita 878, litasafirisha mita bilioni 10 za ujazo za gesi kwa mwaka kutoka Azerbaijan hadi Italia kupitia Ugiriki, Albania na Bahari ya Adriatiki.

Awamu ya kwanza ya gesi hiyo inatazamiwa kuwasili barani Ulaya mwaka 2020 ambapo Ugiriki itafaidika kwa mafao ya kodi kwa miaka 25.

Comments are closed.