AZMA YA ZITTO KUJIUZULU UBUNGE YAGONGA MWAMBA

AZMA YA ZITTO KUJIUZULU UBUNGE YAGONGA MWAMBA

Like
238
0
Friday, 20 March 2015
Local News

AZMA ya Mbunge wa Kigoma Kaskazini ,KABWE ZITTO kupitia CHADEMA,ya kutaka kujiuzulu Ubunge imegonga mwamba baada ya kuelezwa kuwa Spika wa Bunge ,ANNE MAKINDA amemzuia,kufanya hivyo.

ZITTO ambaye alikuwa ameshafanya maandalizi ya kuaga Bunge March 19 ndani ya Bunge,amejikuta akigonga mwamba dakika za mwisho baada ya kuingia Bungeni na kuelezwa na mmoja wa Maofisa wa Bunge kuwa, suala lake la kutoa hotuba limeahirishwa na Spika MAKINDA, akitakiwa kwanza kuifanyia marekebisho.

Kabla kuingia Bungeni,ZITTO alikuwa akibadilishana mawazo na Mwanasheria wake,ALBERT MSANDO,huku akiwa ameshika jalada maalum ambalo ndani yake kulikuwa na hotuba ambayo angeisoma

Comments are closed.