BAADA YA CAF KUITAKA MTIBWA ILIPE DOLA 15,000, UONGOZI WAKE WASEMA HAWAKO TAYARI KULIPA

BAADA YA CAF KUITAKA MTIBWA ILIPE DOLA 15,000, UONGOZI WAKE WASEMA HAWAKO TAYARI KULIPA

Like
507
0
Thursday, 05 July 2018
Sports

Shirikisho la soka nchini (TFF), kupitia kwa Katibu mkuu wake Kidao Wilfred leo wameweka wazi kuwa, wanalishughulikia suala la faini waliyopigwa Mtibwa Sugar na CAF na watahakikisha timu hiyo inashiriki michuano ya Kombe la Shirikisho barani Africa.

Akizungumza na wanahabari leo, Kidao amesema suala la Mtibwa Sugar na faini waliyopigwa na CAF mwaka 2003 ya dola za Kimarekani 15000, wanalifanyia kazi na watajitahidi kuhakikisha faini hiyo inalipwa kabla ya Julai 20 ili timu hiyo iweze kushiriki.

Mwaka 2003, Mtibwa Sugar ilipigwa faini na CAF pamoja na kufungiwa kutoshiriki michuano yoyote inayosimamiwa na shirikisho hilo kwa misimu miwili, kutokana na kushindwa kwenda kucheza mechi ya marudiano dhidi ya Santos FC ya Afrika Kusini katika mchezo wa Kombe la Shirikisho Afrika. Katika mchezo wa kwanza hapa nyumbani Mtibwa Sugar ilifungwa mabao 3-0.

Hata hivyo kwa mujibu wa uongozi wa Mtibwa Sugar wao wanadai wameshalipa faini hiyo, kipindi ambacho Shirikisho la soka lilikuwa linaitwa FAT. Kidao amesema wao kama TFF hawajaziona rekodi hivyo itawalazimu kuwasiliana na CAF ili kujua kama faini hiyo ililipwa.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *