Joe Jackson, Baba wa Michael Jackson amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 89.
Joe ambaye ni baba wa watoto 11 aliwahi pia kuwa Msimamizi wa kundi la muziki la The Jackson 5 amefariki akiwa anapatiwa matibabu huko Las Vegas nchini Marekani akiwa anasumbuliwa na maradhi ya Saratani.
Mtoto wake wa nne, Jermaine, aliiambia Daily Mail kuwa kabla ya kifo baba yake amejaribu kuzuia familia yake isimtembelee huku akizuia habari kuhusu maendeleo ya afya pamoja na eneo alilopo.
Waliruhusiwa kumwona tarehe 19 Juni. “Hakuna mtu aliyejua nini kinachoendelea,” alisema Jackson. “Hatupaswi kuomba kumuona baba yetu, hasa kwa wakati kama huu. Tumekuwa tukiumia sana, alisema Jermaine