BACLEY’S YAKANUSHA KUUZWA

BACLEY’S YAKANUSHA KUUZWA

Like
258
0
Wednesday, 02 March 2016
Local News

BENKI ya Bacley’s Tanzania imekanusha taarifa ambazo sio sahihi juu ya kusitishwa kwa huduma zake kwa madai kuwa Benki hiyo imeuzwa kwa nchi za Afrika.
Akizungumza na Waandishi wa Habari Jijni Dar s salaam jana wakati wa kutoa ripoti ya Benki hiyo kwa kipindi cha mwaka mmoja kwa niaba ya mkurugenzi mkuu wa benki hiyo, mkuu wa idara ya masoko wa Bacley’s JOE BENDERA amesema kuwa Benki hiyo inaendelea kutoa huduma kwa wateja wake kwa ufasaha na inaendelea kuboresha zaidi.
Aidha amebainisha kuwa miongoni mwa mafanikio waliyopata kwa kipindi cha mwaka mmoja ni pamoja na kuwafikia wateja milioni 42 kwa nchi za Afrika na kueleza kuwa wataeendelea kuwafikia watu wengi zaidi ya idadi hiyo.

Comments are closed.