BAJETI ya mwisho kwa Serikali ya awamu ya Nne ya Rais JAKAYA KIKWETE, inatarajiwa kujadiliwa na kuchambuliwa wiki ijayo huku ratiba ya Bunge ya Bajeti ikionesha itajadiliwa kwa siki 44.
Tayari Kamati za Kudumu za Bunge zinatarajia kuanza kuijadili kuanzia April 27 hadi Mei 9 mwaka huu, kabla ya wabunge kuanza kuijadili bungeni.
Taarifa ambayo imeifia Kituo hiki, kutoka Ofisi za Bunge imeeleza kuwa, Kamati hizo zitaichambua Bajeti hiyo inayohitimisha Utawala wa Serikali ya Rais KIKWETE jijini Dar es salaam.