BAKWATA YATHIBITISHA VIFO VYA MAHUJAJI 5 KUTOKA TANZANIA NCHINI SAUDI ARABIA

BAKWATA YATHIBITISHA VIFO VYA MAHUJAJI 5 KUTOKA TANZANIA NCHINI SAUDI ARABIA

Like
516
0
Friday, 25 September 2015
Local News

BAKWATA imethibitisha kutokea kwa vifo vya Watanzania  watano miongoni mwao mmoja ni raia wa Kenya waliofariki huko Minna Saudi Arabia wakati mahujaji wakielekea kwenye Jamaraat , ambako kulikuwa na msongamano mkubwa uliopelekea mahujaji zaidi ya 700 kufariki na mamia kadhaa kujeruhiwa.

 

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo na Sheikh Mkuu wa Tanzania Abu Bakari Zuberi Watanzania waliotambuliwa hadi jana usiku wametajwa kuwa ni Mwanaisha Hassan Juma, Mkungwe Suleiman Hemedi na Sefu Saidi Kitimla na  Mwanamke mwingine mmoja Mtanzania jina halijaweza kupatikana ambapo Raia wa Kenya ametambuliwa kwa jina la Fatuma Mohammed Jama.

 

Aidha taarifa hiyo imeeleza kuwa Kuna taarifa ya mahujaji wanawake wawili ambao hadi Alhamisi usiku walikua hawajapatikana na hivyo kutokuwa na uhakika juu ya usalama wao hadi watakapopatikana.

MAKA MKA

Comments are closed.