MJUMBE wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM, Balozi Seif Ali Iddi, amesema Watanzania wanaoishi Zanzibar na Bara, wataendelea kushirikiana kwa miaka mingi zaidi kutokana na mwingiliano wao wa kidamu.
Balozi Seif Ali Iddi amesema uwepo wa ushirikiano huo ndio njia pekee itakayotoa fursa kwa Watanzania hao kusaidiana katika kutatua changamoto zinazowakabili miongoni mwao na vizazi vyao.
Balozi Iddi ambaye pia ni Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, amesema hayo wakati akizungumza katika mkutano wa ujirani mwema kati ya wanachama wa CCM na viongozi wa Mkoa wa Magharibi, Unguja na kutoka Kata ya Mtoni, Wilaya ya Temeke, jijini Dar es salaam.