BAN KI-MOON ALAANI KUFUKUZWA KWA MRATIBU WA MISAADA YA KIBINAADAMU WA UMOJA WA MATAIFA

BAN KI-MOON ALAANI KUFUKUZWA KWA MRATIBU WA MISAADA YA KIBINAADAMU WA UMOJA WA MATAIFA

Like
272
0
Tuesday, 02 June 2015
Local News

KATIBU Mkuu wa umoja wa mataifa BAN KI-MOON amelaani kufukuzwa kwa mratibu wa misaada ya kibinaadamu wa Umoja wa Mataifa TOBY LANZER huko nchini Sudan Kusini .

Katibu mkuu huyo ameitaka serikali hiyo kubadili uamuzi huo mara moja kwa kuwa  Lanzer alikuwa mstari wa mbele katika kutafuta ufumbuzi wa mahitaji kwa jamii ya nchi hiyo iliyoathiriwa na mzozo kwa kuhakikisha kwamba misaada inawafikia.

Aidha amesema kuwa suala hilo ni muhimu sana hasa kwa wakati huu wa vurugu zinazoendelea kwa pande zote mbili katika vita vya wenyewe kwa wenyewe ambapo hadi sasa vimesababisha vifo kwa maelfu ya watu tangu mwezi disemba mwaka 2013.

Comments are closed.