BAN KI-MOON ATARAJIWA KUANZA ZIARA MASHARIKI YA KATI

BAN KI-MOON ATARAJIWA KUANZA ZIARA MASHARIKI YA KATI

Like
214
0
Wednesday, 21 October 2015
Global News

KATIBU MKUU wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-Moon ataliarifu baraza la usalama la Umoja wa Mataifa leo, kuhusu ziara yake ya Mashariki ya Kati, iliyolenga kutuliza ghasia zilizodumu kwa wiki kadhaa sasa.

 

Ban Ki-Moon alitoa ombi la kuzungumza na baraza hilo haraka kupitia njia ya video, kutokea mji wa Ramallah, uliyoko katika Ukingo wa Magharibi wa Palestina.

 

Katibu mkuu huyo wa Umoja wa Mataifa alifanya ziara ya kustukiza katika eneo hilo jana, ili kutoa onyo kwa pande mbili za Waisrael na Wapalestina, kukomesha vurugu mara moja.

Comments are closed.