BAN KI MOON ATUMA SALAMU ZA PONGEZI KWA MAGUFULI

BAN KI MOON ATUMA SALAMU ZA PONGEZI KWA MAGUFULI

Like
218
0
Wednesday, 11 November 2015
Local News

KATIBU Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki Moon ametuma salamu za pongezi kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa dokta John Pombe Magufuli kwa kuchaguliwa kuwa Rais wa Tanzania wa awamu ya Tano.

 

Katika salamu zake katibu Mkuu huyo amesema kuwa Uchaguzi wa mwaka huu ni uthibitisho wa wazi na dhamira ya muda mrefu ya Watanzania kwa demokrasia, Amani na utulivu.

 

Mbali na hayo Ban Ki Moon amesema anaamini kuwa, chini ya uongozi wa Rais dokta Magufuli, Serikali ya Tanzania itashughulika na juhudi za kuondoa umasikini, kuimarisha utawala bora na kuendeleza juhudi za kupigania Amani na utulivu katika Ukanda wa Afrika Mashariki na nje ya Ukanda huo.

Comments are closed.