BAN KI MOON AWASILI NIGERIA

BAN KI MOON AWASILI NIGERIA

Like
194
0
Monday, 24 August 2015
Global News

KATIBU mkuu wa umoja wa mataifa Ban Ki-moon amewasili jana nchini Nigeria tayari kwa kuanza ziara ya siku mbili nchini humo.

Katika ziara hiyo Ban ki-moon anaitembelea Nigeria kwa lengo la kuwatembelea waathirika wa mashambulizi yaliyofanywa katika ofisi za umoja huo mjini Abuja yanayodaiwa kufanywa na wanamgambo wa Boko Haram miaka minne iliyopita.

Ban Ki Moon pia atakutana na Rais wa Nigeria Muhammadu Buhari ili kujadili namna ya kupambana na vikundi vyenye msimamo mkali ambapo pia anatarajiwa kuwa na mazungumzo na makundi yanayoendesha kampeni za kuwarudisha wasichana wa shule zaidi ya mia mbili waliotekwa na Boko Haram mwaka uliopita.

Comments are closed.