BAN KI-MOON KUANZA ZIARA KOREA KASKAZINI

BAN KI-MOON KUANZA ZIARA KOREA KASKAZINI

Like
177
0
Monday, 16 November 2015
Global News

KATIBU Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-Moon anatarajiwa kufanya ziara nchini Korea Kaskazini, na hivyo kuwa kiongozi wa kwanza wa umoja huo duniani kuizuru nchi hiyo kwa zaidi ya miaka 20 iliyopita.

 

Shirika la habari la Korea Kusini, Yonhap, limesema kuwa Ban atazuru Korea Kaskazini baadae wiki hii, ingawa tarehe kamili bado haijatangazwa.

 

Hata hivyo taarifa kutoka ngazi za juu za Umoja wa Mataifa zimeeleza kwamba Ban alikuwa tayari kukutana na kiongozi wa Korea Kaskazini, Kim Jong-Un, ambaye bado hajampokea kiongozi wa nchi tangu aingie madarakani mwaka 2011 baada ya kifo cha baba yake, Kim Jong-Il. Mwezi Mei mwaka huu.

Comments are closed.