BANZA STONE AFARIKI DUNIA

BANZA STONE AFARIKI DUNIA

Like
338
0
Friday, 17 July 2015
Entertanment

MSANII  mkongwe wa muziki wa dance Tanzania, Ramadhan Masanja maarufu  Banza Stone  amefariki dunia leo mchana baada ya kuugua kwa muda mrefu.

Akizungumza na efm kwa njia ya simu, kaka wa Marehemu Jabir Masanja amethibitisha kutokea kwa msiba huo na kwamba taratibu zote zinafanyika nyumbani kwao Sinza jijini Dar es salaam.

Kwa mujibu wa ndugu wa marehemu, Banza alikuwa anasumbuliwa na fangasi waliokuwa wanamshambulia kichwani (ubongo) na shingoni.

EFM  inatoa pole kwa ndugu jamaa na marafiki na Wapenzi wa Muziki wa Dansi nchini Tanzania.

Mwenyezi Mungu ailaze roho ya marehemu mahali pema peponi. AMEN

 

Comments are closed.