BARABARA YA GARDEN-GARDEN AVENUE KUBADILISHWA JINA LEO

BARABARA YA GARDEN-GARDEN AVENUE KUBADILISHWA JINA LEO

Like
437
0
Thursday, 30 October 2014
Local News

 

BARABARA ya Garden-Gardern Avenue iliyopo katikati ya Jiji la Dar es salaam inatarajia kuitwa Barabara ya Humburg kuanzia leo.

Taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya Habari imeeleza kuwa Meya wa Jiji la Dar es salaa Dokta DIDAS MASABURI anatarajiwa kuwa miongoni mwa wageni watakaoshiriki tukio hilo la Kihistoria la kubadilisha jina.

Mbali na Dokta MASSABURI wengine watakaohudhuria hafla hiyo ni pamoja na Diwani Mkuu wa Jimbo la Humburg nchini Ujerumani WOLFGANG SCHMIT na Balozi wa Heshimia anaeiwakalisha Tanzania jijini humo PETRA HAMMELMAM.

Taarifa zaidi zimebainisha kuwa hatua ya kubadilisha jina mbayo litaanza kutumika rasmi leo imelenga kuakisi ushirikiano baina ya Majiji hayo mawili ya Dar es salaam na Hurmburg.

 

Comments are closed.