BASI LA AIR JORDAN LAPATA AJALI MTU MMOJA AFARIKI DUNIA

BASI LA AIR JORDAN LAPATA AJALI MTU MMOJA AFARIKI DUNIA

Like
572
0
Wednesday, 15 April 2015
Local News

MTU mmoja amefariki Dunia, na wengine ishirini kujeruhiwa kufuatia ajali iliyohusisha basi kampuni ya Air Jordan na gari ndogo  baada ya kuacha njia na kuanguka katika eneo la migua wilaya ya Nzega mkoani Tabora.

Efm imezungumza na kamanda wa mkoani humo Suzan Kaganda, amesema kuwa chanzo cha awali cha kutokea kwa ajali hiyo kinaonesha ni mwendo kasi wa basi hilo ambalo lilikuwa likitokea jijini Mwanza kuelekea jijini Dar es salaam.

Kamanda Kaganda ameeleza kuwa hadi sasa maiti imeshatambuliwa na ndugu wa marehemu ambapo majeruhi wote wa ajali wapo katika hospitali ya Nzega mkoani humo.

AIR33

AIR22

Comments are closed.