BBC KUTOA TUZO YA MCHEZAJI BORA AFRIKA

BBC KUTOA TUZO YA MCHEZAJI BORA AFRIKA

Like
467
0
Tuesday, 11 November 2014
Slider

Wachezaji watano watajwa kuweza kuwania tuzo ya mchezaji bora wa bara la Afrika inayotolewa na Shirika la utangazaji habari nchini Uingereza (BBC).

Wachezaji waliopata nafasi ya kuingia katika kiny’ang’anyiro hicho ni Yaya Toure (Ivory Coast, Man City), Yacine Brahimi (Algeria, Porto), Vicent Enyeama (Nigeria, Lille), Gervinho (Ivory Coast, Roma) na Pierre Emerick Aubameyang (Gabon, Borussia Dortmund).

Tuzo hiyo inayoshikiliwa na mchezaji wa timu ya Taifa ya Ivory Coast na klabu ya Man City, Yaya Toure inatoa nafasi kwa mashabiki wa soka kuweza kumchanga mchezaji wanayemtaka kwa kupiga kura kwa njia ya mtandao au kwa kutumia simu ya kiganjani.

Mchakato wa kupiga kura utaendeshwa mpaka tarehe 24 mwezi Nov huku mshindi kutangazwa mnamo tarehe 1 mwezi Desemba mwaka 2014.

Comments are closed.