BESIGYE AKAMATWA TENA

BESIGYE AKAMATWA TENA

Like
282
0
Monday, 22 February 2016
Global News

KIONGOZI wa chama cha upinzani cha Forum for Democratic Change (FDC) nchini Uganda Kizza Besigye amekamatwa tena na maafisa wa polisi nchini humo.

Watu walioshuhudia kukamatwa kwake wamesema kwamba Kizza amekamatwa alipokuwa akijaribu kuondoka nyumbani kwake alipokuwa amewekwa kizuizini.

Awali kulikuwa na habari kwamba kiongozi huyo angefika makao makuu ya Tume ya Uchaguzi kuonesha matokeo rasmi ya uchaguzi wa urais ingawa tayari Tume ya Uchaguzi ilishamtangaza Rais Yoweri Museveni kuwa mshindi wa uchaguzi wa urais uliofanyika Alhamisi wiki iliyopita.

Comments are closed.