BILIONI 8 KUPANUA UWANJA WA NDEGE MWANZA

BILIONI 8 KUPANUA UWANJA WA NDEGE MWANZA

Like
441
0
Thursday, 20 November 2014
Local News

UJENZI kwa ajili ya upanuzi wa Uwanja wa Ndege wa Mwanza unaendelea kwa kasi baada ya serikali kulipa kiasi cha fedha kwa mkandarasi.

Imeelezwa kuwa Serikali imeshatoa Shilingi Bilioni Nne kwa Mkandarasi ambaye ni Kampuni ya BCEG ya China.

Ukarabati unaofanywa ni upanuzi wa Uwanja wa kuongeza njia za kurukia ndege, jengo la kuongozea ndege na ghala la mizigo.

Kiasi hicho cha fedha kinafanya fedha ambazo serikali imeshamilipa Mkandarasi kufikia Shilingi Bilioni 13. Meneja wa Uwanja huo ESTHER MADALE amesema kazi ya upanuzi wa Uwanja huo inaendelea vyema na kwa kasi.

 

 

 

Comments are closed.