Binti wa miaka 7 amburuza baba yake mzazi polisi

Binti wa miaka 7 amburuza baba yake mzazi polisi

Like
618
0
Thursday, 13 December 2018
Global News

Binti wa miaka saba nchini India amemshitaki baba yake polisi baada ya kushindwa kutekeleza ahadi aliyomuahidi.

Hanifa Zaara amewambia polisi kuwa baba yake “amemdanganya” na anatakiwa akamatwe.

Hanifa Zaara amewaambia polisi kuwa baba yake “amemdanganya” na anatakiwa akamatwe na kushtakiwa.

Ahadi yenyewe ni ya kujengewa choo, binti huyo amesema anaona aibu kwenda haja vichakani kwa kukosa choo.

Wahindi wengi hawana vyoo na takribani watu milioni 500 huenda haja nje, kwa mujibu wa shirika la Unicef.

Barua ya Hanifa kwa polisi

Hata kwa baadhi ya wenye vyoo, hawavitumii na badala yake kujisaidia nje.

Hanifa amabaye anaishi na wazazi wake katika mji wa Ambur, jimboni Tamil Nadu, hajawahi kuona choo nyumbani kwao.

Ameiambia BBC kuwa ni majirani wachache tu ndio ambao wana vyoo majumbani. Hivyo akiwa shule ya chekechea alimuomba baba yake kujenga choo, naye akakubali.

“Nilikuwa nikijisikia aibu kwenda kujisaidia nje huku watu wakiniangalia,” amesema Hanifa. Alipata zaidi ari ya kuwa na choo baada ya kujifunza shule madhara ya kiafya ya kujisaidia nje.

Katika barua aliyoiandikia polisi, amesema baba yake alimuahidi kumjengea choo iwapo ataongoza darasani.

“Nimekuwa nikiongoza darasani toka nikiwa chekechea. Nipo darasa la pili sasa. Kila siku anasema atajenga. Huu ni uongo, hivyo tafadhali mkamateni.”

Hata kama si kukamatwa, binti huyo aliwataka polisi wamlazimishe kusaini barua itakayoeleza lini atajenga choo hicho.

Baba yake, Ehsanullah, ameiambia BBC kuwa alishaanza kujenga choo hicho, lakini kwa sasa hana pesa ya kukikamilisha. Baba huyo hana ajira kwa sasa.

“Nilimuomba Hanifa anipe muda zaidi lakini amegoma kuongea nami kwa sababu sijamtimizia ahadi yake,” aliongeza.

Lakini Hanifa hajamuelewa baba yake. “Mpaka lini nitamuomba baba yangu kitu hicho hicho? Amekuwa akinipa kisingizio hicho cha kutokuwa na pesa kila siku. Hivyo nikaenda polisi.”

Jumatatu alikwenda kituo cha polisi karibu na shule anayosoma akiongozwa na mama yake, Mehareen.

Choo ambacho baba wa Hanifa alianza kujenga lakini hakijakamilika

“Amekuja na begi lililojaa vyeti vya ubora wa ufaulu wake shuleni akavitandaza mezani kwangu,” afisaa wa polisi A Valarmathi BBC Tamil. “Akaniuliza, je waweza kunipa choo?”

Polisi ikabidi impigie simu baba mzazi wa binti huyo ambae aliharakisha polisi akidhani familia yake ipo kwenye matatizoni.

Baada ya kufika polisi alipigwa na butwaa kujua sababu ya kuitwa kwake.

“Sikudhani jambo hili lingenigeukia kwa namna ambayo limegeuka,” amesema.

Kilio cha Hanifa kiliungwa mkono na polisi ambao pia waliwashirikisha viongozi wa wilaya ambao sasa wanachangisha pesa za kujenga vyoo 500 kwenye eneo ambalo anaishi binti huyo.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *