BIRDMAN AKANA KUHUSIKA NA JARIBIO LA KUTAKA KUMUUA LIL WAYNE

BIRDMAN AKANA KUHUSIKA NA JARIBIO LA KUTAKA KUMUUA LIL WAYNE

Like
217
0
Friday, 24 July 2015
Entertanment

Birdman amevunja ukimya kufuatia tuhuma zinazo muhusisha yeye na Young Thug kuhusika na jaribio la kutaka kumuua Lil Wayne.

Birdman amekana kuhusika kwa aina yoyote kupanga njama za mauaji licha ya maelezo ya polisi kumtuhumu yeye na Young Thug.

Chanzo cha karibu na Wayne na Birdman kilizungumza na mtandao wa Tmz juu ya taarifa zinazosambazwa na zinazodaiwa kutolewa na polisi kuwa Birdman alipokea simu April 26, ikiwa ni muda mfupi baada ya basi maalum la show la Lil Wayne kutupiwa risasi huko Atlanta Birdman alipokea simu kutoka kwenye eneo la tukio.

Simu hiyo inasemekana imepigwa na mtu aliyekuwa kwenye kambi ya Wayne lakini mtu huyo hakufahamika na kwa maelezo ya simu hiyo ilikuwa ikimpa taarifa Birdman juu ya kile kilichotokea  kabla ya tukio

Chanzo hiki kimeeleza kuwa Birdman amemuhakikishia Lil Wayne kuwa hakusika na tukio hilo na kuapa kusaidia kumsaka aliyehusika au wahusika.

Akijibu juu ya simu iliyosajiliwa kwa jina lake Birdman amesema haimshangazi kwakuwa hizo ni simu za kampuni hivyo zinatumiwa na wengi

Comments are closed.