BLATTER ANAWANIA URAIS FIFA

BLATTER ANAWANIA URAIS FIFA

Like
301
0
Friday, 29 May 2015
Slider

RAIS  wa shirikisho la soka duniani- FIFA, Sepp Blatter,anagombea kiti cha urais katika uchaguzi wa shirikisho hilo unaotarajiwa kufanyika leo huko Zurich Uswisi.

Uchaguzi huo unaendelea katika kongamano la kila mwaka la shirikisho hilo licha ya shinikizo kutoka kwa wadau Blatter ajiondoe kufuatia tuhuma za ufisadi na ulaji rushwa katika shirikisho hilo uliopelekea maafisa wakuu saba kukamatwa mapema juma hili.

Blatter anakabiliwa na upinzani mkali kutoka kwa mwana mfalme kutoka Jordan Ali Bin al Hussein.

 

Comments are closed.