BODI YA SUKARI IMETAKIWA KUSHUGHULIKIA MADAI YA WAKULIMA WADOGO WA MIWA KILOMBERO

BODI YA SUKARI IMETAKIWA KUSHUGHULIKIA MADAI YA WAKULIMA WADOGO WA MIWA KILOMBERO

Like
288
0
Tuesday, 24 November 2015
Local News

KATIBU Mkuu Wizara ya Kilimo, Chakula na Ushirika Bi. Sophia Kaduma ameiagiza Bodi ya Sukari nchini, kushughulikia haraka madai ya wakulima wadogo wa miwa katika Kiwanda cha Sukari cha Kilombero Mkoani Morogoro ili kuleta usawa.

Katika Agizo hilo, Katibu Mkuu huyo ameiagiza Bodi hiyo kukutana na Uongozi wa Kiwanda  cha Sukari cha Kilombero na  ule wa wakulima wadogo wa miwa ili kupata ufumbuzi wa kudumu kuhusu soko la miwa wanayozalisha.

 

Aidha, Katibu Mkuu ametoa muda wa siku saba kwa Bodi ya Sukari Tanzania iwe imeshatekeleza na kutoa taarifa ya utekelezaji wa agizo hilo.

Comments are closed.