BODI ya Usajili wa Wahandisi nchini Tanzania –ERD, imefanikiwa kutengeneza ajira elfu 1,600 kwa Watanzania kufuatia usajili wa kampuni 160 ya ushauri wa kihandisi zilizoanzishwa kote nchini katika kipindi cha miaka 10 kuanzia mwaka 2005 hadi 2015.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es salaam kuelezea mafanikio ya Bodi hiyo kwa kipindi cha miaka 10, Msajili wa Wahandisi nchini, Muhandisi Steven Mlope amesema kuwa kwa kusajili kampuni 160 katika kipindi cha miaka 10 pia wamefanikiwa kusajili wahandisi wapatao elfu 8,496 ambao kwa ujumla wao wametengeneza ajira kwa Watanzania 256,480.