BODI YA UTALII IMETAKIWA KUTUMIA VYOMBO VYA HABARI VYA KIMATAIFA KUITANGZA TANZANIA

BODI YA UTALII IMETAKIWA KUTUMIA VYOMBO VYA HABARI VYA KIMATAIFA KUITANGZA TANZANIA

Like
247
0
Thursday, 07 January 2016
Local News

WAZIRI wa Maliasili na Utalii Profesa Jumanne Maghembe ameitaka Bodi ya Utalii Tanzania- TTB, kuendelea kutumia vyombo vya habari vya Kimataifa kama vile CNN na BBC  kuitangaza Tanzania kama eneo la Utalii duniani sambasamba na kuweka makala na matangazo ya utalii katika majarida ya Kimataifa yanayoandika habari za Utalii na usafiri (Travel Magazine) ambayo ndiyo husomwa na watalii wengi duniani.

Waziri Maghembe amesema hatua hiyo itasaidia kuongeza idadi ya watalii nchini.

 

Waziri Maghembe ameyasema hayo alipotembelea Bodi ya Utalii Tanzania na kukutana na Menejimenti  ya TTB kwa lengo la
kujitambulisha na kubadilishana mawazo kuhusu utekelezaji wa majukumu ya Bodi katika utangazaji utalii ndani na nje ya nchi.

Comments are closed.