BODI YA UTALII KUFANYA MAONYESHO DAR

BODI YA UTALII KUFANYA MAONYESHO DAR

Like
194
0
Thursday, 09 July 2015
Local News

BODI ya utalii nchini  imesema inatarajia kufanya maonyesho ya utalii Jiji Dar es salaam ambayo  yanategemea kuanza mapema mwezi wa kumi mwaka huu .

Akizungumza na Kituo hiki, Kaimu Mkurugenzi mwendeshaji bodi ya utalii Tanzania DEVOTHA MDACHI amesema kuwa maandalizi kwa ajili ya maonyesho ya utalii ya meshaanza na bodi inategemea kupokea mawakala wa utalii zaidi ya 50 na wanahabari wasiopungua 10 kutoka Mataifa mbali mbali.

Amebainisha kuwa, maonyesho  hayo ni nafasi kubwa kwa wafanyabiashara  wa Tanzania kutangaza kazi zao za kisanii na kukuza  soko la utalii nchini hali itakayosaidia kuinua uchumi wa nchi.

Comments are closed.