BODI YA WATAALAMU WA UNUNUZI NA UGAVI YATOA MAFUNZO KWA WAALIMU

BODI YA WATAALAMU WA UNUNUZI NA UGAVI YATOA MAFUNZO KWA WAALIMU

Like
252
0
Monday, 16 February 2015
Local News

BODI ya Wataalam wa Ununuzi na Ugavi imeendesha mafunzo kwa walimu ,Wataalam wanaosimamia Wanafunzi wa Fani ya Ununuzi na Ugavi wanaofanya tafiti kama sehemu ya mafunzo yao ya Stashahada ya ununuzi na ugavi.

Mafunzo hayo yamefunguliwa na mjumbe wa bodi ya Wakurugenzi, AZIZ KILONGE, ambaye amewaasa Wataalam hao kuhakikisha kwamba wanasimamia Wanafunzi kwa Ukamilifu ili kuongeza ubora wa kazi za utafiti zinazofanywa.

Amefafanua kuwa uzingatiaji wa Maadili katika kufanya tafiti, ndio msingi na matakwa ya Bodi, ili kuhakikisha kuwa wanafunzi wanafanya tafiti na sio kuchukua kazi zilizofanywa na Wanafunzi ama watafiti wengine au kufanyiwa na watu wengine.

Comments are closed.