WATOTO 30 wametekwa nyara na watu wanaodhaniwa kuwa wapiganaji wa Boko Haram.
Watoto hao wametekwa nyara kaskazini mashariki mwa Nigeria.
Tukio hili linakuja siku chache baada ya kundi hilo kuwateka wanawake na wasichana kaskazini mashariki mwa nchi hiyo.
Hadi sasa wasichana wa shule 200 waliotekwa na wanamgambo hao miezi tisa iliyopita bado hawajulikani walipo.