BOKO HARAM WAVAMIA KIJIJI NA KUUA 15

BOKO HARAM WAVAMIA KIJIJI NA KUUA 15

Like
350
0
Wednesday, 31 December 2014
Global News

 WAPIGANAJI wanaodhaniwa kuwa ni Boko Haram wamevamia kijiji Kaskazini Mashariki mwa Nigeria na kuua watu takriban 15.

Shambulizi hilo limetokea kijiji cha Kautikari katika jimbo la Borno, pale washukiwa wa Boko Haram walipowasili kijijini humo kwa magari yenye silaha, wakilenga Askari wa Ulinzi wa Jadi wa mji huo.

Kijiji hicho kipo karibu na Chibok mahali ambapo kundi la Boko Haram, limewatekanyara Wasichana wa shule zaidi ya 200 mwezi Aprili mwaka huu.

Comments are closed.