KUNDI la jihad lililoko Nigeria, Boko Haram, kwa mara ya kwanza limeishambulia Chad.
Wakuu nchini humo wanasema kuwa, wapiganaji wa Boko Haram walivuka ziwa Chad kwa maboti usiku na kushambulia kijiji cha Ngouboua, kilichoko kandokando ya ziwa hilo.
Majeshi ya Chad yanasemekana kuwarudisha nyuma wapiganaji hao ambao wanadhibiti eneo kubwa la ziwa hilo upande wa Nigeria.