BOKO HARAM YASHAMBULIA KASKAZINI MASHARIKI MWA NIGERIA

BOKO HARAM YASHAMBULIA KASKAZINI MASHARIKI MWA NIGERIA

Like
229
0
Friday, 07 August 2015
Global News

WAASI wa kundi la kigaidi la Boko Haram wamewaua kwa bunduki watu wasiopungua tisa katika vijiji viwili Kaskazini Mashariki mwa Nigeria.

 

Wanakijiji wameelezea namna ambavyo watu waliokuwa wamebeba silaha walivyowasili kwa pikipiki na kuvamia kijiji chao. Wanamgambo walipora mali kwenye nyumba na maduka na kisha kuzichoma moto nyumba zilizokuwa zimeezekwa kwa nyasi.

 

Shambulio hili limewalazimisha mamia ya wakazi wa eneo hilo kukimbilia mji wa Potiskum uliopo kilomita 70 kutoka nyumbani kwao.

 

Comments are closed.