WAPIGANAJI wa kundi la kigaidi la Boko Haram wamewateka nyara watu zaidi ya 60 baada ya kufanya shambulio kaskazini mwa nchi jirani ya Cameroon.
Kwa mujibu wa taarifa ya polisi, magaidi hao walifanya shambulio hilo hapo jana, yaani siku moja baada ya Chad kuwapeleka wanajeshi wake nchini Cameroon, ili kupambana na magaidi hao.
Afisa mmoja wa polisi ameliambia shirika la habari la AFP kwamba, wapiganaji wa Boko Haram walivivamia vijiji viwili vya kaskazini mwa Cameroon hapo jana na walizichoma moto nyumba na kuwateka nyara watu wasiopungua 60.