BOMOABOMOA KUANZA KINONDONI

BOMOABOMOA KUANZA KINONDONI

Like
338
0
Tuesday, 17 November 2015
Local News

MANISPAA ya Kinondoni kwa kushirikiana na Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, kama msimamizi na mtekelezaji wa sera ya Taifa ya Ardhi, inakusudia kuendesha zoezi la kubomoa nyumba zilizojengwa bila kufuata taratibu za ujenzi.

 

Sera ya Taifa ya Ardhi imebainisha sababu inayosababisha Wizara kushirikiana na Manispaa ya Kinondoni kuendesha zoezi hilo la ubomoaji kwa kuhusisha nyumba zote zilizojengwa Bila kibali cha ujenzi na Bila kufuata michoro ya mipango miji

 

Maeneo ambayo ujenzi wake umekiuka matumizi yaliyokusudiwa na yatahusika na ubomoaji huo ni Mbezi, Tegeta, Bunju, Mwenge na Kinondoni–Biafra ambapo Kazi hiyo inatarajiwa kufanyika kwa siku tatu kuanzia kesho Novemba 18 hadi Novemba 20 mwaka huu.

Comments are closed.