BOMU LA KUTEGA LAUA WANNE SOMALIA

BOMU LA KUTEGA LAUA WANNE SOMALIA

Like
310
0
Monday, 05 January 2015
Global News

WATU WANNE wameuwawa katika shambulizi la bomu lililotegwa kwenye gari karibu na Uwanja wa ndege wa Kimataifa katika mji Mkuu wa Somalia, Mogadishu.

Afisa wa Polisi amesema mshambuliaji amegongesha gari lililosheni mabomu na gari jingine na kusababisha mlipuko ulioutikisa mji wa Mogadishu na kusikika katika maeneo mengine ya mji huo.

Msemaji wa Kitengo cha Kijeshi cha kundi la Al Shabab lenye mafungamano na mtandao wa Kigaidi wa Al Qaeda, Sheikh ABDUL AZIZ MUSAB amethibitisha wanamgambo wa kundi hilo kufanya hujuma hiyo.

Comments are closed.