BOMU LA KUTEGWA LAUA WATU KADHAA SYRIA

BOMU LA KUTEGWA LAUA WATU KADHAA SYRIA

Like
263
0
Thursday, 22 January 2015
Global News

WATU wasiopungua sita wameuawa katika mlipuko wa bomu lililokuwa limetegwa kwenye gari katika mji wa Homs katikati mwa Syria.

Gari hiyo ililipuka katika eneo lenye makazi ya watu na maduka katika kitongoji cha Akrama, ambacho kimekuwa kikishambuliwa mara kwa mara kwa sababu kinaonekana kuwa nyumbani kwa watu wa jamii ya Alawi ambao ni wafuasi wa rais wa Syria Bashar al Assad.

Gavana wa mji wa Homs Talal Barrazi amethibitisha idadi ya vifo vilivyotokea akisema wengi walikuwa wanawake na watoto. Watu wengine 30 walijeruhiwa katika hujuma hiyo.

 

 

Comments are closed.