BOTI ILIYOKAMATWA NA MIHADARATI KUSAMBARATISHWA KENYA

BOTI ILIYOKAMATWA NA MIHADARATI KUSAMBARATISHWA KENYA

Like
233
0
Friday, 14 August 2015
Global News

SERIKALI ya Kenya inatarajiwa kuharibu boti moja iliyopatikana imebeba takriban kilo 7 za mihadarati aina ya Heroini.

Boti hiyo inayoitwa ‘Baby Iris’ ilikamatwa na polisi kwa tuhuma za ulanguzi wa mihadarati katika bahari ya Kenya huko Mombasa na itaharibiwa kulingana na sheria za Kenya.

Ripoti ya polisi inasema kuwa ‘Baby Iris’ inamilikiwa na bwenyenye mmoja raia wa Uingereza na kwamba Jeshi la wanamaji la Kenya ndilo lililokabidhiwa jukumu hilo la kuiharibu.

Comments are closed.