BOTI YA UVUVI YA URUSI YAZAMA, WATU ZAIDI YA HAMSINI WAHOFIWA KUFA MAJI

BOTI YA UVUVI YA URUSI YAZAMA, WATU ZAIDI YA HAMSINI WAHOFIWA KUFA MAJI

Like
319
0
Thursday, 02 April 2015
Global News

BOTI ya uvuvi ya Urusi imezama katika visiwa vya Kamchatka , ikiwa na mabaharia wapatao hamsini na wanne ambao inadhaniwa kuwa wamekufa maji wote.

Watu wapatao sitini na watatu wameopolewa ambao nao walikuwa ndani ya boti hiyo ya uvuvi,wengine wamekumbwa na homa ya mapafu na wengine kumi na watano wameripotiwa kuwa hawaonekani.

Taarifa za awali zinasema kwamba kabla meli hiyo ya uvuvi haijazama ilikuwa na watu wapatao miamoja na thelathini na mbili ,Wengi wao walikuwa wanatokea maeneo ya Vanuatu, Latvia na Ukraine na nahodha ni miongoni mwa waliopoteza maisha.

Comments are closed.