BRN YAKABILIWA NA CHANGAMOTO KATIKA SEKTA YA ELIMU

BRN YAKABILIWA NA CHANGAMOTO KATIKA SEKTA YA ELIMU

Like
315
0
Friday, 23 January 2015
Local News

KUFUATIA utafiti uliofanywa na Hakielimu na kutoa Takwimu zinazoonesha   kushuka kwa Elimu kwenye baadhi ya Mikoa nchini ikiwemo Mkoa wa Rukwa Kantalamba jimbo la Nkasi ambapo hali ya utekelezaji wa malengo ya Matokeo Makubwa Sasa si ya kuridhisha bado Sekta ya Elimu imeonesha kuwa na changamoto kubwa mkoani humo.

Akizungumza na Efm mara baada ya utafiti huo kutolewa mbunge wa jimbo la Nkasi Mheshimiwa Ally Kessy amesema siyo kweli kwamba elimu haijafanikiwa kwenye jimbo hilo kwakuwa Shule zimekuwa nyingi na Waalimu wasomi wamekuwa wengi pia.

Mpango wa Matokeo Makubwa Sasa ulipanga kuongeza kiwango cha ufaulu kwa shule za msingi na sekondari kufikia asilimia 60 hadi mwaka 2013 jambo ambalo limeonesha kuwa changamoto licha ya ongezeko la ufaulu kukuwa bado azma hiyo imefanikiwa kwa asilimia 79 na 42 tu kwa shule za sekondari na msingi.

 

Comments are closed.