BUDAPEST: SAFARI ZA TRENI KWA WAHAMIAJI ZASITISHWA

BUDAPEST: SAFARI ZA TRENI KWA WAHAMIAJI ZASITISHWA

Like
195
0
Tuesday, 01 September 2015
Global News

KITUO kikuu cha reli cha kimataifa mjini Budapest leo kimeamuru kuondolewa kwa mamia ya wahamiaji wanaojaribu kupanda treni kuelekea Austria na Ujerumani.

Tangazo la kipaza sauti lililotolewa hadharani limesema hakuna treni zitakazoondoka au kuwasili katika kituo hicho cha Keleti hadi hapo itakapotolewa taarifa zaidi na kwamba kila mtu alitakiwa aondoke katika kituo hicho.

Kwa mujibu wa shirika la habari la AFP tangazo hilo linakuja baada ya wahamiaji 500 wanaume,  wanawake na watoto kujaribu kupanda treni ya mwisho kuelekea Austria.

Comments are closed.