BUHARI ATUA CAMEROON KUIMARISHA NGUVU YA KUPAMBANA NA BOKO HARAM

BUHARI ATUA CAMEROON KUIMARISHA NGUVU YA KUPAMBANA NA BOKO HARAM

Like
273
0
Thursday, 30 July 2015
Global News

RAIS wa Nigeria Muhammadu Buhari ameanza ziara ya siku mbili nchini Cameroon na akiwa huko analenga kuboresha mahusiano na nchi jirani na pia kuimarisha ushirikiano katika kupambana na wanamgambo wa Boko Haram.

 

Buhari alipokelewa na mwenzake wa Cameroon, Paul Biya katika uwanja wa kimataifa wa mji mkuu  Yaounde.mbali na mazungumzo yao ya jana,  Viongozi hao watakutana na waandishi wa habari leo.

 

Nigeria, Niger, Cameroon na Chad zimeungana katika kuwapiga waasi wa Boko Haram ambao sasa wamekuwa tishio hata nje ya Nigeria.

 

Comments are closed.