BUJUMBURA: WAANDAMANAJI WACHOMA MOTO BASI

BUJUMBURA: WAANDAMANAJI WACHOMA MOTO BASI

Like
257
0
Monday, 25 May 2015
Local News

BASI  moja limechomwa moto mjini Bujumbura Burundi na waandamanaji waliorejea mabarabarani kupinga uamuzi wa rais Pierre Nkurunziza kuwania muhula wa tatu.

Kitongoji cha Kanyosha kimekuwa kitovu cha maandamano hayo dhidi ya awamu ya tatu ya rais Nkurunziza.

Maandamano haya yanarejea baada ya kuuawa kwa kiongozi wa chama cha upinzani Zedi Feruzi nje ya nyumba yake katika mji mkuu Bujumbura.

 

Comments are closed.