BUNGE LA 11 LAANZA KUJADILI HOTUBA YA RAIS

BUNGE LA 11 LAANZA KUJADILI HOTUBA YA RAIS

Like
300
0
Tuesday, 26 January 2016
Local News

MKUTANO wa pili wa Bunge la 11 umeanza leo mjini Dodoma ambapo Bunge la Jamhuri ya Muungano linajadili hotuba ya Rais kwa muda wa siku tatu aliyoitoa wakati wa ufunguzi wa Bunge hilo. Kikao cha kwanza cha Bunge hilo kimeanza kwa kipindi cha maswali na majibu ambapo baadhi ya wabunge wamepata nafasi ya kuiuliza maswali serikali na kuhoji mikakati mbalimbali inayotarajiwa kufanywa kwa manufaa ya Taifa. Awali kabla ya kipindi cha maswali na majibu kuanza, Spika wa Bunge mheshimiwa Job Ndugai amewaapisha baadhi ya wabunge ambao walikuwa bado hawajaapishwa.

Comments are closed.