BUNGE LA 11 LAENDELEA NA ZOEZI LA KIAPO CHA UAMINIFU KWA WABUNGE

BUNGE LA 11 LAENDELEA NA ZOEZI LA KIAPO CHA UAMINIFU KWA WABUNGE

Like
387
0
Wednesday, 18 November 2015
Local News

BUNGE la kumi na moja la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania limeendelea leo kwa kikao cha pili kinachoenda sambamba na zoezi la Kiapo cha Uaminifu kwa wabunge wote.

Hiyo imekuja baada ya jana Bunge hilo kufanikiwa kumpata Spika Mheshimiwa Jobu Ndugai atakayeliongoza kwa kipindi cha miaka mitano.

Mheshimiwa Ndugai alishinda nafasi hiyo baada ya kupata jumla ya Kura 254 kati ya 365 zilizopigwa na wabunge wote ambayo ni sawa na asilimia 70.

Comments are closed.